Michuano ya Ligi ya Muungano ambayo ilirejea rasmi msimu uliopita, inatarajiwa kuanza kutimua vumbi April 23 visiwani Zanzibar
Kulingana na ratiba, April 23 michuano hiyo itaanza kutimua vumbi kuanzia robo fainali kwa mchezo kati ya JKU dhidi ya Singida Black Stars
April 24, Zimamoto itachuana na Coastal Union huku KMKM ikichuana na Azam Fc. Yanga itashuka dimbani Ijumaa, April 25 kumenyana na KVZ
Klabu za Yanga, Azam Fc, Coastal Union na Singida Black Stars ndizo zinazoiwakilisha Tanzania Bara huku JKU, Zimamoto, KMKM na KVZ zikiiwakilisha Zanzibar
