International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi April 17 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
17 Apr 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi April 17 2025

Klabu ya Ligi kuu ya Pro ya Saudi, Al-Nassr, inamtaka kiungo wa Chelsea na timu ya taifa ya Ecuador, Moises Caicedo, 23, ambaye anatarajiwa kugharimu zaidi ya Β£100m. (Telegraph)

Juventus imemfanya kiungo wa Italia mwenye umri wa miaka 24 anayechezea Newcastle, Sandro Tonali, kuwa miongoni mwa wachezaji inayowataka katika uhamisho wa majira ya joto. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

RB Leipzig inatarajiwa kuweka bei ya Β£86m kwa mshambuliaji wa Slovenia, Benjamin Sesko, 21, ambaye anavivutia vilabu vya Manchester United, Chelsea na Arsenal. (Bild)

Tottenham itakataa ofa kwa ajili ya beki wake wa kushoto raia wa Italia, Destiny Udogie, 22, katika majira haya ya joto licha ya kuhusishwa na klabu kadhaa ikiwemo Manchester City. (Florian Plettenberg)

Sporting iko tayari kupokea ofa za majira ya joto kwa ajili ya beki wa Ureno mwenye umri wa miaka 23, Goncalo Inacio, ambaye ananyatiwa na Manchester United. (A Bola)

Benfica inataka kumsajili tena mshambuliaji wa Ureno mwenye umri wa miaka 25 wa Chelsea, Joao Felix, ambaye yuko kwa mkopo AC Milan. (Record)

Juventus inataka kuongeza muda wa mkopo wa beki wa Ureno mwenye umri wa miaka 21, Renato Veiga, anayetokea Chelsea. Inataka ama kwa mkopo mwingine au kwa uhamisho wa kudumu wa Β£48m. (Tuttosport)

Klabu ya MLS, Chicago Fire, imefanya mawasiliano kumsajili kiungo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 33 wa Manchester City, Kevin de Bruyne, ambaye ataondoka mkataba wake utakapokamilika katika majira ya joto. (Fabrizio Romano)

Mshambuliaji wa England, Marcus Rashford, 27, anatumai kiwango chake kilichoimarika akiwa kwa mkopo Aston Villa kitavutia timu bora za Ulaya, huku klabu yake mama Manchester United ikiwa haitaki kumrudisha katika majira ya joto. (Talksport)

Manchester United tayari imeanza kuandaa orodha fupi ya wachezaji wanaoweza kumrithi Rashford, huku Aston Villa ikiwa haijui kama itatumia fursa ya kuweza kumsajili kwa uhamisho wa kudumu utakaogharimu Β£40m. (Sky Sports)

Mshambuliaji mkongwe wa zamani wa Ufaransa, Antoine Griezmann, 34, yuko tayari kuongeza mkataba wake na Atletico Madrid hadi Juni 2027 licha ya uvumi kuwa anaweza kuhamia MLS. (Mundo Deportivo)

Kiungo wa Liverpool, Ryan Gravenberch, haondoki Anfield hivi karibuni licha ya wakala wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi kuzungumzia uwezekano wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kuchezea Real Madrid. (Mail)

Mshambuliaji wa West Ham, Michail Antonio, 35, anakabiliwa na wakati mgumu kusubiri kuona kama ataongezewa mkataba na klabu hiyo huku mchezaji huyo wa Jamaica akitarajiwa kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu. (Times )

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’