Local,Normal News,Simba, Stellenbosch

CAF CC : Simba dhidi ya Stellenbosch leo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
20 Apr 2025
CAF CC : Simba dhidi ya Stellenbosch leo

Katika kile kinachotarajiwa kuwa mchezo wa kuvutia na wenye ushindani mkali, Simba SC ya Tanzania inawakaribisha wageni kutoka Afrika Kusini, Stellenbosch FC, kwenye uwanja wa kihistoria wa New Amaan Complex kwa ajili ya mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF (CAF Confederation Cup)

Ni mechi kubwa na muhimu kwa Simba kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga fainali ya michuano hiyo na kurudia kile walichofanya mwka 1993

Wakicheza mechi ya Kimataifa kwa mara ya kwanza visiwani Zanzibar, Simba inatarajiwa kupata sapoti kubwa ya mashabiki ambapo dimba la New Amaan Complex linatarjiwq kuwa 'full house'

Kwa kuwa ni mechi ambayo Simba inahitaji kushinda nyumbani, Kocha Fadlu Davids ni wazi ataingia na mfumo wake wa kushambulia, akimtegemea mshambuliaji Steven Mukwala kuongoza mashambulizi

Mganda huyo atasaidiana na Elie Mpanzu, Kibu Denis, na Jean Charles Ahoua huku eneo kati likitarajiwa kuwa chini ya usimamizi wa viungo Fabrice Ngoma na Yusuf Kagoma

Safu ya ulinzi itaendelea kuwa imara ikiongozwa na wazoefu Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Abdulrazak Hamza, na Carabou Chamou, huku Simba wakitarajiwa kutumia kwa ustadi faida ya kucheza nyumbani

Hata hivyo ni wazi haitakuwa mechi nyepesi kwani licha ya Stellenbosch kuwa wageni wapya kwenye michuano ya kimataifa, wamewashangaza wengi kwa kiwango chao bora msimu huu

Timu hiyo ya Afrika Kusini imeonesha ubora mkubwa, hasa walipowang'oa mabingwa watetezi Zamalek katika hatua ya robo fainali – kitendo kilichowafanya kuchukuliwa kwa uzito mkubwa sasa

Simba leo inapaswa kumaliza mechi nyumbani kwa kuibuka na ushindi mnono ili kuwa na kazi rahisi ya kukamilisha mpango wa kutinga fainali pale watakaposafiri Afrika Kusini kwa mechi ya marudiano wiki ijayo

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
43m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’