Local,Normal News,Simba, Stellenbosch

Simba yaichapa Stellenbosch bao 1-0 nusu fanali CAF CC

Joel JJ By Joel JJ
β€’
20 Apr 2025
Simba yaichapa Stellenbosch bao 1-0 nusu fanali CAF CC

Bao la dakika ya 45 kipindi cha kwanza kupitia mpira wa adhabu kutoka kwa Jean Charles Houa limetosha kuipa Simba ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya Stellenbosch katika mchezo wa mkondo wa kwanza nusu fainali ya kombe la Shirikisho (CAC CC)

Ulikuwa mchezo wa vipindi viwili, Simba ilitawala na kutengeneza nafasi nyingi katika kipindi cha kwanza huku Stellenbosch wakicheza kwa kujihami zaidi na kutumia mashambulizi ya kushitukiza

Kipindi cha pili mkufunzi wa Simba Fadlu Davids alibadili mbinu akiwaacha Stellebosch kumiliki mchezo huku Simba ikitumia mashambulizi ya kujibu

Kulikuwa na nafasi ya Simba kumaliza mchezo dakika za majeruhi lakini Ahoua alishindwa kutumia nafasi adimu ambayo ni wazi ingeweza kuifanya Simba iende Afrika Kusini kwenye mchezo wa pili ikiwa na ushindi mnono zaidi

Pengine mashabiki walitamani ushindi wa mabao mengi lakini hii ni nusu fainali na katika hatua hii hakuna timu dhaifu

Simba itakuwa katika nafasi nzuri ya kusonga mbele hatua ya fainali endapo itashinda mchezo wa marudiano au sare yoyote na zaidi itakuwa na faida kubwa kama itafunga bao la ugenini

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’