Local,Normal News,Yanga, Fountain

Yanga yaipania Fountain Gate NBC PL

Joel JJ By Joel JJ
β€’
21 Apr 2025
Yanga yaipania Fountain Gate NBC PL

Kuelekea mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya Fountain Gate dhidi ya Yanga ambao utapigwa leo Jumatatu, April 21 katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa Manyara, Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amesema wamejipanga kushinda mchezo huo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa

Aidha Hamdi ambaye ameiongoza Yanga katika mechi 11 akishinda 10 na kutoka sare mechi moja, amesema amekiandaa kikosi chake kimbinu kuikabili Fountain Gate

Amesema anaamini wachezaji wake watatafsiri vyema mpango wa mchezo huo na kuibuka na ushindi

"Lazima tuwe makini sana, tushinde kila mechi. Pia, tumefanya mikutano ya kiufundi, tumeangalia video na kufanya mazoezi ya kiufundi ili kujiandaa vizuri"

"Ninawaambia mara nyingi nyota wa mchezo ni mfumo. Wachezaji wote wakielewa mfumo, tutashinda mechi nyingi. Tuna wachezaji wenye uwezo wa kufanya mfumo ufanye kazi lakini jambo la kwanza ni kuelewa mfumo"

"Kwa hiyo mchezaji anapobadilishwa au kuingia uwanjani, lazima ajue moja kwa moja anachotakiwa kufanya na kile asichopaswa kufanya na kuelewa wa Wachezaji wangu naamini tutaendelea kufanya vizuri kwenye kila mchezo," alisema

Aidha, Hamdi amekiri baadhi ya wachezaji wake wana changamoto za majeruhi na maumivu ya hapa na pale lakini amesema yeye anaamini ana timu imara na ataendelea na utaratibu wa kumpa nafasi kila mchezaji

"Ni kweli tuna baadhi ya wachezaji majeruhi kama Aucho, Pacome bado hajawa tayari, Musonda anahisi maumivu kidogo si makubwa lakini hatuwezi kumuhatarisha pamoja na Azizi Ki ana maumivu ya muda mrefu"

"Nawaheshimu wachezaji wote. Mimi si kocha wa kulalamika kwamba sina huyu au yule hapana nitampa nafasi kila mchezaji. Hiyo ndiyo njia pekee ambayo itatuwezesha kufika mwezi Mei tukiwa imara, kwa sababu kila mchezaji atakuwa amepewa muda wa kucheza. Hilo ni jambo muhimu sana kwangu," aliongeza Hamdi

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
46m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’