Baada ya kupoteza mchezo kwa kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union hapo jana, klabu ya KenGold imekuwa timu ya kwanza kushuka msimu huu
Baada ya kushuka dimbani mara 27, KenGold imekusanya alama 16 tu, huku ikiwa na mechi 3 zilizosalia kuhitimisha msimu
Kama itashinda mechi zote, itafikisha alama 25 ambazo tayari klabu ya Prisons inayoshika nafasi ya 14 imezipita
Prisons ina alama 27 sawa na Pamba Jiji inayoshika nafasi ya 13 lakini ikiwa bado na mechi nne
Kagera Sugar nayo iko hatarini ikishika nafasi ya 15 na alama zake 22
Kagera Sugar itahitaji kushinda mechi zote tatu zilizosalia huku ikiomba dua baya kwa wapinzani wake wasishinde mechi zao
