International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa April 25 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
25 Apr 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa April 25 2025

Arsenal imepiga hatua katika mazungumzo ya kumsajili kiungo wa kati wa Real Sociedad na Uhispania Martin Zubimendi, 26, ambaye ana kipengele cha kutolewa cha euro milioni 60 sawa na (pauni milioni 51.2)

katika kandarasi yake. (ESPN) Manchester United inaweza kumtoa mshambuliaji wa Denmark Rasmus Hojlund, 22, kwa Atalanta badala ya mshambuliaji wa Nigeria Ademola Lookman, 27(Sun)

Roma, Napoli na vilabu viwili vya ligi ya Premea vina nia ya kumsajili winga wa Nottingham Forest wa Uingereza Callum Hudson-Odoi, 24, ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao. (Sky Sports)

Newcastle ina nia ya kutumia kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 30 katika mkataba wa mshambuliaji wa Ipswich na England wa Chini ya miaka 21 Liam Delap, 22, ambacho kitaanza kuzingatiwa ikiwa Tractor Boys watashushwa daraja kutoka Ligi ya Premia. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Wolves Matheus Cunha, 25, yuko tayari kujiunga na Manchester United, ambao wamedhamiria kukamilisha dili la Mbrazili huyo msimu huu wa joto. (Sky Germany)

Tottenham Hotspur itaanza mazungumzo kuhusu kandarasi mpya ya beki wa Argentina Cristian Romero, 26, ambaye anafuatiliwa na Real Madrid na Atletico Madrid. (CaughtOffside)

Atletico Madrid pia wana nia ya kumsajili kiungo wa Tottenham mwenye umri wa miaka 27 na Uruguay Rodrigo Bentancur. (Times)

Kiungo wa Ubelgiji Albert Sambi Lokonga, 25, amepata majeraha manne akichezea Sevilla kwa mkopo msimu huu na anatazamiwa kurejea Arsenal msimu wa kiangazi, huku klabu hiyo ya La Liga ikipania kutumia kumsajili kwa Β£10.25m. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Manchester City na Ubelgiji Kevin de Bruyne, 33, hatacheza Kombe la Dunia la Vilabu la Fifa mwezi Juni kwa kuhofia kuumia na kuhatarisha utafutaji wake wa klabu mpya. (Daily Star)

Tottenham Hotspur wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na Uingereza Marcus Rashford, 27, kwa mkataba wa kudumu msimu huu wa joto. (Football transfer)

Wawakilishi wa mshambuliaji wa Real Madrid na Brazil Vinicius Jr wanakanusha kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anakaribia kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. (Athletic)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’