Kikosi cha Yanga kimeondoka jijini Dar es Salaam leo Ijumaa kwenda visiwani Zanzibar kwa ajili ya ushiriki wa michuano ya Kombe la Muungano 2025 iliyoanza jana
Yanga imepangwa kuvaana na KVZ kesho Jumamosi katika mchezo wa robo fainali ya michuano hiyo iliyorejeshwa msimu uliopita
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ametamba kuwa hawaendi kushiriki tu michuano hiyo, bali dhamira yao ni kurejea na kombe Dar es salaam
"Tunawaambia tu, wenyeZanzibar yetu tinakuja, msimu huu tumesema hatuachi kitu," alitamba Kamwe
Michuano hiyo inafanyika kisiwani Pemba katika uwanja wa Gombani ambapo jana JKU ilitangulia nusu fainali baada ya ushindi wa mikwaju ya penati 6-5 baada ya matokeo ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Singida Black Stars
Mechi mbili zinatarajiwa kupigwa leo ambapo Zimamoto itachuana na Coastal Union na KMKM wakichuana na Azam Fc