International,Normal News,Liverpool, Tottenham

Liverpool wamebeba premia mapema tu

Joel JJ By Joel JJ
28 Apr 2025
Liverpool wamebeba premia mapema tu

Jana Liverpool ilijihakikishia ubingwa wa ligi kuu ya Premia mapema baada yha kuibamiza Totenham Hotspur kwa mabao 5-1 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Anfield.

Liverpool sasa wanakuwa mabingwa wa ligi ya juu England wakifikisha makombe 20 sawa na Manchester United.

Totenham ilianza kutangulia kupitia bao la kona lililofungwa na Dominic Solanke dakika ya 12, kisha Luiz Diaz ameweka sawa mzani kwa kumalizia pasi safi ya Dominic Szoboszlai dakika ya 16 na baadaye Alexis MacAllister dakika ya 24akapiga shuti kali lililomuacha kipa Guglielmo Vicario mdomo wazi alipogeuka na kukuta nyavu zikitikisika.

Furaha ya mashambiki wa Liverpool walioujaza Uwanja wa Anfield yalipomwagwa majivu ya lejendari Billy Shanky iliongezeka baada ya Mholanzi Cody Gakpo dakika ya 34 kupigilia msumari kisha kuvua fulana na kuonyesha iliyokuwa ndani iliyoandikwa ‘Welcome to Jesus’ (karibu kwa Yesu). Gakpo amepigwa kadi ya njano kutokana na tukio hilo.

Mohammed Salah hakubaki mbali na goli la Totenham baada ya kuifungia Liveepool bao la nne dakika ya 62 na kukikaribia kiatu cha mfungaji bora wa EPL msimu huu kwa kufikisha mabao 28 kisha kuibua shangwe kwa mashabiki aliopiga nao ‘selfie’.

Dakika ya 68’, mchezaji wa Totenham, Destiny Udogie amekoleza furaha kwa mashambiki wa Liverpool baada ya kujifunga.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE →
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE →
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE →
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE →
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE →
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE →
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE →
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE →
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE →
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE →