Jana kigogo mwingine kutoka Tanzania Bara Azam Fc aliaga michuano ya ligi ya Muungano akikubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa JKU katika mchezo wa nusu fainali
Kipigo hicho kimezfanya timu tatu kutoka Tanzania Bara Singida BS, Coastal Union na Azam Fc kuaga michuano hiyo inayofanyika Gombani, Pemba
Yanga ndio timu pekee iliyobaki kutoka Bara na leo itashuka dimba la Gombani kumenyana na Zimamoto katika mchezo wa pili wa nusu fainali utakaopigwa sa 1:15 usiku
JKU ambayo iliziondoa Singida BS na Azam Fc, tayari imetinga fainali ikisubiri mshindi wa mchezo wa leo kuelekea mechi fainali
Je Yanga itafanikiwa kwenda fainali leo au itaungana na wawakilishi wengine wa Bara kuaga michuano hiyo mapema?



