Local,Normal News,Simba, Mashujaa

Simba yaipania Mashujaa Fc

Joel JJ By Joel JJ
β€’
1 May 2025
Simba yaipania Mashujaa Fc

Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola amesema timu iko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mashujaa Fc ambao utapigwa kesho Ijumaa, May 02 katika uwanja wa KMC Complex

Akizungumza katika Mkutano na wanahabari mapema leo, Matola alisema wanatambua kila mchezo uliobaki kwenye ligi una umuhimu mkubwa katika kutimizamalengo ya msimu huu

Hivyo wanauchukulia mchezo huo kama fainali na dhamira iliyopo ni kuchukua alama zote tatu

Amesema wanatambua Mashujaa Fc sio timu nyepesi lakini wana imani kwenye ubora wa kikosi na hivyo matarajio ni kuchukua alama zote tatu

"Tumekuwa na maandalizi mazuri kuelekea mchezo huu. Tunauchukulia mchezo huu kama fainali kwani tunajua tunahitaji kushinda"

"Licha ya ubora wa Mashujaa Fc, lakini tunaamini tutakuwa bora zaidi yao na kwenda kupata alama tatu kama malengo yetu yalivyo," alisema Matola

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, kiungo Awesu Awesu amesema ari na morali kila mchezaji iko juu

Wanakwenda kucheza mechi hii kama walivyofanya katika mechi zilizopita na muhimu ni kuhakikisha alama zote tatu zinabaki Msimbazi

"Wachezaji wote tuko tayari, morali ya timu iko juu kuelekea mchezo huu. Tunauchukulia mchezo huu kwa uzito uleule kama mechi iliyopita"

"Namaini kwa maandalizi tuliyofanya, tutacheza vizuri na kuibuka na ushindi," alisema Awesu

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
44m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’