Yanga imefanikiwa kunyakua taji la Muungano baada ya kuichapa JKU bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliopigwa uwanja wa Gombani, Pemba
Bao pekee la Yanga katika mchezo huo lilifungwa na Maxi Nzengeli katika kipindi cha kwanza akimalizia pasi murua kutoka kwa Farid Mussa
Ni rekodi kwa Yanga kushinda taji hilo kwa mara ya saba tangu kuanzishwa kwake mwaka 1982
Kiungo Mudathir Yahya ameibuka mchezaji bora wa michuano hiyo huku Maxi Nzengeli akiibuka mchezaji bora mchezo wa fainali huku pia akiibuka mfungaji bora wa mashindano