Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa michezo (CAS) imelitupilia mbali shauri lililofunguliwa na Yanga dhidi ya TFF na Bodi ya Ligi baada ya kuahirishwa mechi namba 184 dhidi ya Simba iliyopaswa kupigwa March 08 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
CAS imeitaka Yanga kuhakikisha inakamilisha taratibu zote za rufaa katika mamlaka za ndani
Kulingana na taarifa ya CAS, Yanga walipaswa kufungua madai yao TFF na kama wasingeridhika na maamuzi ndio wangekata rufaa CAS na hivyo watalazimika kuanza upya mchakato kwa kufuata utaratibu huo
Tayari Bodi ya Ligi (TPLB) imetangaza kuendelea na maandalizi ya mechi za mwisho wa msmu pamoja na maboresho ya ratiba ikiwa ni pamoja na kuupangia tarehe mchezo namba 184