International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa May 2 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
2 May 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa May 2 2025

Newcastle wanamtaka mshambuliaji wa Brentford na Cameroon Bryan Mbeumo, mwenye umri wa miaka 25, lakini wana wasiwasi kuhusu ada yake ya uhamisho ya Β£60m. (Telegraph)

Newcastle pia hawatakuwa na nia ya kumfuatilia kwa muda mrefu beki wa kati wa Bournemouth Dean Huijsen, mwenye umri wa miaka 20, baada ya kujifunza kutokana na juhudi za mwaka jana za kushindwa kumsaini beki wa England Marc Guehi, mwenye umri wa miaka 24 kutoka Crystal Palace. (i paper)

Arsenal wanaweza kukabiliana na ushindani kutoka Paris St-Germain kumsaini beki wa Roma kutoka Ivory Coast Evan Ndicka, mwenye umri wa miaka 25, ambaye thamani yake iko kati ya Β£25-34m. (Mirror)

Manchester United wanataka kumsajili beki wa kati wa Ujerumani Jonathan Tah, mwenye umri wa miaka 29, majira ya kiangazi baada ya mkataba wake kumalizika na Bayer Leverkusen. (Sky Sports)

Chelsea hawana mpango wa kumuuza kiungo wao kutoka Argentina Enzo Fernandez, mwenye umri wa miaka 24, aliyesajiliwa kwa rekodi ya Β£107m, ambaye pia anafuatiliwa kwa muda mrefu na Real Madrid. (Sky Sports)

Manchester United wamekubaliana kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa Enzo Kana-Biyik, mwenye umri wa miaka 18 kutoka Le Havre. (Fabrizio Romano)

Bayer Leverkusen wanataka kumzuia kiungo mshambuliaji wa Ujerumani Florian Wirtz kujiunga na Bayern Munich majira haya ya kiangazi, huku Manchester City na Real Madrid pia wakivutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Sky Germany)

Real Madrid wako tayari kumruhusu kipa wa Ukraine Andriy Lunin, mwenye umri wa miaka 26, kuondoka msimu huu, huku kipa wa Chelsea Kepa Arrizabalaga, Mhispania mwenye umri wa miaka 30, kwa sasa akiwa mkopo Bournemouth, akizingatiwa kuwa mbadala wake. (Mundo Deportivo)

Aston Villa wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, mwenye umri wa miaka 33, ambaye ataondoka Manchester City mwishoni mwa msimu. (Football Insider)

Crystal Palace watataka zaidi ya Β£80m kama wataamua kumuuza kiungo wa England Adam Wharton, mwenye umri wa miaka 21, majira haya ya kiangazi. (Teamtalk)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’