Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola amesema ratiba ni ngumu lakini wako tayari kukabiliana na kila changamoto inayokuja mbele yao ili kuwapa furaha mashabiki wa timu hiyo
Leo Jumatatu, Simba itakuwa dimbani pale Isamuhiyo, Mbweni jijini Dar es salaam kuikabili JKT Tanzania katika mechi nyingine ngumu ya ligi kuu
Ni siku tatu tu zimepita tangu Simba ikabiliane na Mashujaa Fc katika mchezo ambao Simba iliibuka na ushindi katika dakika za lala salama
Matola amesema wanatambua mechi dhidi ya JKT Tanzania haitakuwa nyepesi lakini wana wajibu wa kudhihirisha ukubwa wa klabu ya Simba kwa kushinda mechi ngumu
"Tunaifahamu vyema JKT Tanzania sio timu nyepesi kwa sababu ina wachezaji wengi wenye uzoefu wa ligi kuu"
"Ni kweli ratiba ni ngumu, kucheza kila baada ya siku tatu sio jambo jepesi kwa wachezaji lakini sisi kama Simba ni timu kubwa, tuko tayari kukabiliana na changamoto yoyote inayokuja mbele yetu," alisema Matola



