International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu May 05 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
5 May 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatatu May 05 2025

Manchester United yajiunga na kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Cameroon ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa pauni milioni 60 Bryan Mbeumo, 25, kutoka Brentford msimu huu wa kiangazi. (Telegraph - usajili unahitajika)

Arsenal wanamfuatilia mshambuliaji wa Brazil Rodrygo anayekipiga Real Madrid, huku Manchester City pia wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Relevo - kwa Kihispania)

Manchester City pia wanapanga kuendeleza nia yao ya kufikia makubaliano na Nottingham Forest kwa ajili ya kiungo wao wa kati wa Uingereza Morgan Gibbs-White, 25. (Fabrizio Romano)

Arsenal na Aston Villa wanamtaka mshambuliaji wa Juventus Dusan Vlahovic, 25, huku klabu hiyo ya Serie A ikitarajiwa kuitisha pauni milioni 42 kwa Mserbia huyo. (Fichajes - kwa Kihispania)

Everton iko tayari kumenyana na Manchester United ili kuinasa saini ya mshambuliaji wa Ipswich Muingereza Liam Delap, 22. (Teamtalk)

Manchester United iko tayari kuwasilisha dau la kumsajili mlinzi wa Barcelona na Uruguay Ronald Araujo, 26, ikiwa itafuzu kwa Ligi ya Mabingwa. (Football365)

Leeds imemuorodhesha beki wa Marseille na Argentina Leonardo Balerdi, 26, kuwa mmoja wa shabaha yao wakuu wa uhamisho wa majira ya kiangazi. (Sun)

Real Madrid iliwapeleka waska vipaji wao kuwafuatilia beki wa Bournemouth na Uhispania Dean Huijsen, 20, na beki wa Hungary Milos Kerkez, 21, wakati wa mechi yao ya Jumamosi dhidi ya Arsenal. (TBR Football)

Miamba hao wa Uhispania pia wanamnyatia beki wa Arsenal na Ufaransa William Saliba, 24, ambaye kandarasi yake na The Gunners inaendelea hadi 2027. (L'Equipe - kwa Kifaransa)

West Brom inamtaka kocha wa Tottenham Muingereza Ryan Mason, 33, kuwa meneja wao mpya. (Sun)

Mkufunzi wa Fulham Mreno Marco Silva, 47, atawania kuchukua nafasi ya Ange Postecoglou katika klabu ya Tottenham ikiwa raia huyo wa Australia mwenye umri wa miaka 59 atatimuliwa baada ya klabu hiyo kuandikisha matokeo mabaya msimu huu. (Football Insider)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
44m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’