Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza msimamo kuwa hawatoshiriki mchezo namba 184 wa ligi kuu dhidi ya Simba kutokana na ukiukwaji wa kanuni uliopelekea mchezo huo kutofanyika Machi 08
Licha ya maelekezo ya Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa Michezo (CAS) kuwataka wafungue upya madai yao katika mamlaka za ndani kabla ya kuyawasilisha kwenye chombo hicho cha juu zaidi, Yanga imeeleza kukosa imani na wenye mamlaka kuwa hawako tayari kutenda haki kwa klabu hiyo
Hivyo Yanga imesisitiza itaendelea kuipigania haki yake kwa njia nyingine ili kukomesha dhurma na uvunjaji mkubwa wa kikanuni unaofanywa na Mamlaka ya soka kwa maslahi mapana ya maendeleo ya soka



