Simba imeendelea 'kutafuna' viporo vyake leo ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo uliopigwa uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo
Bao pekee la ushindi kwa upande wa Simba lilifungwa na Fabrice Ngoma akimalizia krosi ya Steven Mukwala katika dakika za nyongeza kipindi cha kwanza
Ilikuwa mechi nzuri yenye ushindani, Simba ikitengeneza nafasi zaidi lakini umakini wa mlinda lango wa JKT Tanzania ilikuwa changamoto kwa Mnyama kufunga mabao zaidi
Ushindi huo unaifanya Simba ifikishe alama 63 ikiwa na mechi nyingine mbili za viporo mkononi dhidi ya Pamba Jiji utapigwa May 08 katika uwanja wa KMC Complex kisha kusafiri mkoani Tabora kuikabili KMC May 11