Sio tu kutolewa kwenye mashindano ikiwa katika hatua ya makundi, Ngorongoro Heroes haijafunga bao lolote kwenye mashindano ya Afcon U20 yanayoendelea huko Misri
Ngorongoro Heroes imecheza mechi nne na kupoteza zote. Mechi zote imefungwa bao 1-0 dhidi ya Afrika Kusini, Sierra Leone, Zambia na Misri
Imemaliza kundi A ikishika mkia bila kuwa na pointi yeyote. Huku Afrika kusini ikiongoza kwa pointi 7, ikifuata Sierra Leone kwa pointi 7, Misri 7 na Zambia ikiambulia pointi 6
Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kufuzu kwa michuano hiyo ngazi ya vijana umri chini ya miaka 20
Imewahi kufuzu pia kwa michuano ya U17
