Local,Normal News,Azam

Taoussi apiga hesabu tiketi ya CAF CC

Joel JJ By Joel JJ
โ€ข
10 May 2025
Taoussi apiga hesabu tiketi ya CAF CC

Kocha Mkuu wa Azam FC, Rachid Taoussi amesema matokeo mabaya iliyopata timu hiyo katika mechi za hivi karibuni za Ligi Kuu Bara ni moja ya sababu za kuwarejesha haraka kambini wachezaji ili kujiandaa na mechi tatu za kufungia msimu zitakazoamua hatma yao ya CAF.

Azam, iliyongโ€™olewa mapema katika Ligi ya Mabingwa Afrika iliyoshiriki msimu huu ikiwa ni mara yake ya pili baada ya kuicheza mwaka 2015, lakini haipo katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara wala Kombe la Shirikisho (FA) ilikotolewa raundi ya 32 na Mbeya City.

Jambo hilo limeifanya timu hiyo kusaliwa na tumaini pekee la kukata tiketi ya CAF kwa msimu ujao kwa kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu inayoiwania na Singida Black Stars, jambo linalompa presha kocha Taoussi aliyesema amewaita mapema kambili wachezaji na kuzungumza nao juu ya kufanya kila linalowezekana kumaliza vyema mechi zilizosalia.

Azam imekabiza mecchi tatu dhidi ya Dodoma jiji iliyopangwa kupigwa Mei 13, kabla ya kuvaana na Tabora United na kumalizana na Fountain Gate zitakazopigwa kati ya Juni 18 na 22 kuhitimisha msimu, huku ikisikilizia pia matokeo ya Singida ambayo ipo nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (FA).

Akizungumza na Mwanaspoti, Taoussi alisema hawajatimiza lengo hata moja msimu huu katika michuano waliyoshiriki, hivyo kilichobaki ni kutumia vizuri dakika 270 ili waweze kukusanya pointi tisa zitakazowafanya waendele kusalia katika nafasi ya tatu, huku wakiiombea mabaya Singida iliyopo nyuma yao.

Singida imebakiza mechi nne ikiwamo kiporo dhidi ya Simba na kama ikishinda zote itavuna pointi 12 ambazo ukijumlisha na 53 ilizonazo zitaifanya ifikishe 65, mbili zaidi ya zinazoweza kufikiwa na Azam yenye 54 kwa sasa, ambayo ina mechi tatu mkononi na ikizishinda itafikisha pointi 63 tu.

"Ni kweli hatuna matokeo mazuri baada ya kuenguliwa katika mataji yote tuliyowania msimu huu, nimewaita vijana wangu kambini haraka ili kujiweka tayari kwa mechi tatu zilizobaki. Haitakuwa rahisi, ila mipango inaendelea kusukwa na wachezaji wanatambua kazi tuliyonayo," alisema Taoussi na kuongeza;

"Wapinzani wanaotufukuzia nafasi ya tatu tumewaacha kwa pointi moja hii sio nzuri kwetu licha ya kuanza kwa ushindani mzunguko wa pili tumedondosha pointi nyingi na ndio wa lala salama hivyo mikakati ni kuhakikisha hatudondoshi pointi hata moja kwenye mechi tatu zilizobaki japo haitakuwa rahisi"

Taoussi alisema katika mechi tano zilizopita za ligi wamepoteza pointi sita wakifungwa mechi mbili na kukusanya tisa baada ya kushinda tatu wanahitaji matokeo mechi tatu ili kuwa na mwendelezo wa mechi nne mfululizo kujiweka kwenye nafasi nzuri ya ushiriki kimataifa Kombe la Shirikisho Afrika.

"Ni ligi tu ndio itatupa uwakilishi Shirikisho hivyo tunahitaji kuwekeza nguvu zaidi ili tupate uwakilishi huo wachezaji wanatambua umuhimu wa kupata matokeo kwenye michezo hiyo mitatu na tumekaa na kupanga mikakati njia gani tunafaa kupita ili tufikie malengo"

Mwanaspoti

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
45m ago
READ MORE โ†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE โ†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE โ†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE โ†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE โ†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE โ†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE โ†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE โ†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE โ†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE โ†’