Local,Normal News,Simba, KMC

Simba yalia ya ugumu wa ratiba NBC PL

Joel JJ By Joel JJ
β€’
11 May 2025
Simba yalia ya ugumu wa ratiba NBC PL

Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola amesema wamejipanga kuibuka na ushindi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC ambao utapigwa leo Jumapili katika uwanja wa KMC Complex licha ya ratiba ngumu inayowakabili

Akizungumza katika Mkutano na wanahabari jana, Matola alisema wamekosa muda wa kutosha wa maandalizi ya mechi kutokana na ratiba inayowalazimu kucheza kila baada ya siku tatu

Matola amesema wanajivunia kuwa na kikosi kipana kwani licha ya mabadiliko wanayofanya katika kila mechi, wameendelea kuibuka na ushindi

"Ratiba yetu ni ngumu kwani hatupati muda wa kutosha wa maandalizi lakini tuna kikosi kipana ambacho kinatuwezesha kupata ushindi popote"

"Tunafahamu mchezo dhidi ya KMC utakuwa mgumu lakini sisi tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo chanya," alisema Matola

Simba leo inacheza mechi ya nne katika kipindi cha siku 10 ikishinda mechi tatu zilizopita dhidi ya Mashujaa Fc (2-1), JKT Tanzania (1-0) na Pamba Jiji (5-1)

Baada ya mchezo dhidi ya KMC, Simba itasafiri Morocco kumenyana na RS Berkane katika mchezo wa mkondo wa kwanza fainali ya kombe la Shirikisho (CAF CC) utakaopigwa May 17

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
3m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
32m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’