Mabao mawili ya Steven Mukwala yametosha kuihakikishia ushindi muhimu wa mabao 2-1 dhidi ya KMC katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa KMC Complex
Ulikuwa mchezo wa nne wa kiporo kwa Simba ikikamilisha ratiba ngumu ndani ya siku 10 na kukusanya alama 12, ikifunga mabao 10 na kuruhusu mabao 3
Mnyama alilazimika kutoka nyuma kupata ushindi huo baada ya KMC kutangulia kufunga bao la uongozi mapema katika kipindi cha kwanza
Mukwala akafunga kila kipindi na kuipa Simba alama tatu huku mwenyewe akisogea juu katika mbio za ufungaji bora baada ya kufikisha mabao 11
Simba imefikisha alama 69 sasa ikiwa jino kwa jino na watani zao Yanga ambao wana alama 70 huku tmu zote zikishuka dimbani mara 26
Kwa sasa Simba inaelekeza nguvu zake kwenye fainali ya kombe la Shirikisho (CAF CC) dhidi ya RS Berkane



