Ligi Kuu inaendelea, mechi mbili kupigwa leo

Joel JJ By Joel JJ β€’ 12th May 2025


Ligi Kuu inaendelea, mechi mbili kupigwa leo

Mechi raundi tatu za mwisho ligi kuu ya NBC zinaanza kupigwa leo ambapo Tanzania Prisons na Kagera Sugar zitakuwa nyumbani katika mechi muhimu

Prisons itaikabili Coastal Union katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Sokoine huku Kagera Sugar ikiwa mwenyeji wa Mashujaa Fc

Prisons inayoshika nafasi ya 14 ikiwa na alama 27 inahitaji kushinda leo ili kuweka hai matumaini ya kubaki ligi kuu huku Kagera Sugar inayoshika nafasi ya 15 ikihitaji ushindi pekee ili kuwa nafasi ya kuendelea kupambania maisha kwenye ligi

Endapo Prisons itashinda na Kagera Sugar kukosa ushindi leo ni wazi wana nkurukumbi hao wataungana na KenGold kucheza Championship msimu ujao


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.