Local,Normal News,Simba

Simba yaja na kaulimbiu ya fainali TUNABEBA

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 May 2025
Simba yaja na kaulimbiu ya fainali TUNABEBA

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amesema malengo ya Simba ni kutwaa kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) na wanakwenda kwenye mechi mbili za fainali dhidi ya RS Berkane wakiwa na kauli mbiu ya TUNABEBA

May 17 Simba itakuwa Morocco katika fainali ya kwanza itakayopigwa uwanja wa Manispaa ya Berkane na mchezo wa marudiano utapigwa jijini Dar es salaam. May 25 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Akizungumza katika mkutano na wanahabari mapema leo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali alisema wanasimba wanapaswa kuwa tayari na kila mmoja afahamu safari hii Simba inabeba kombe la Shirikisho baada ya kulikosa mwaka 1993 ilipocheza fainali wakati huo likiitwa kombe la CAF

"Baada ya kumalizana na Berkane ugenini, Mnyama atarudi nyumbani kwa mchezo wa marudiano na kombe litakuwepo Uwanja wa Mkapa. Kuelekea mechi zetu za fainali tunakwenda na kauli mbiu ya TUNABEBA. Tunamaanisha ubingwa wa Afrika safari hii tunabeba. Kuanzia sasa kila Mwanasimba aiweke moyoni hiyo na aanze kufanyia kazi kuhakikisha kombe hili tunabeba."

"Kikosi kitaondoka kesho saa 11 alfajiri kwenda Morocco. Itakuwa safari ya masaa 7 saba moja kwa moja kutoka Dar es Salaam hadi Casablanca. Kwa hili hatuna budi kumshukuru sana, tena kumshukuru tena, tena kumshukuru mara elfu, kumshukuru pakubwa Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wetu wa Tanzania. Kwa hili ametutendea kubwa sana."

"Mpinzani tunayekwenda kucheza nae sio wa kawaida. Hatuhofii rekodi yake wala ubora aliokuwa nao. Tunasema hii TUNABEBA lakini haitakuwa nyepesi, lazima tufanye kazi kwelikweli. Katika hili naomba niseme hii ni vita yetu wote Wanasimba"

"Mechi hii ni ngumu tupambane wote, kila Mwanasimba kwenye eneo lake akampambane anavyoweza. Twendeni vitani, twendeni tukahangaike ili tuchukue ubingwa huu. Tunataka ubingwa, hatuko tayari kwa mara ya pili kwa namna yoyote ile kombe lipo uwanjani akaondoka nalo mwarabu, Simba hatuko tayari," alisema Ahmed

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
46m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’