Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limeagiza mchezo wa mkondo wa pili fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) kati ya Simba dhidi ya RS Berkane kupigwa uwanja wa New Amaan Complex badala ya uwanja wa Benjamin Mkapa
Changamoto ya mvua ndio inayotajwa kuwa sababu ya maamuzi hayo ya CAF baada ya kufanyika ukaguzi wa dimba la Benjamin Mkapa hasa katika kipindi cha mvua
Simba ilishaanza maandalizi kuelekea mchezo huo katika dimba la Mkapa ambapo hata mauzo ya tiketi tayari yalishaanza
Jitihada zinaendelea kwa uongozi wa Simba, TFF na Serikali ambao ndio wamiliki wa dimba la Mkapa kuishawishi CAF ili mchezo huo upigwe kwa Mkapa
Kuna maboresho makubwa yamefanyika tangu ulipofungwa baada ya mchezo dhidi ya Al Masry na CAF wenyewe wlijiridhisha unaweza kutumika