International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa May 16 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 May 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa May 16 2025

Arsenal wanasaka mshambuliaji na wameelekeza macho yao kwa Benjamin Sesko wa RB Leipzig na Slovenia mwenye umri wa miaka 21, au Viktor Gyokeres wa Sporting na Sweden mwenye umri wa miaka 26. (Independent)

Newcastle wanamfuatilia winga wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 20, Jamie Gittens, na pia wanaweza kumsajili kipa mwenzake wa Uswisi, Gregor Kobel mwenye umri wa miaka 27. (Mail)

Liverpool wanaamini Florian Wirtz atasalia Bayer Leverkusen au kujiunga na Bayern Munich, lakini watajaribu kumsajili iwapo kiungo huyo mshambuliaji wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 22 ataamua kuondoka Bundesliga. (Times)

Mshambuliaji mkongwe wa England Jamie Vardy ataondoka Leicester City msimu huu wa joto lakini hana mpango wa kustaafu na anaamini bado anaweza kucheza Ligi Kuu. (Sky Sports)

Mazungumzo mapya kati ya Bayern Munich na beki wa Ufaransa Dayot Upamecano, mwenye umri wa miaka 26, yameanza kuhusu mkataba mpya hadi 2030. (Sky Germany)

Lazio itailipa Arsenal ada ya euro milioni 9 (Β£7.57m) kumsaini beki wa kushoto wa Ureno, Nuno Tavares mwenye umri wa miaka 25. (Fabrizio Romano)

Mshambuliaji wa Manchester United na Denmark, Rasmus Hojlund, mwenye umri wa miaka 22, anakabiliwa na hali ya kutokuwa na uhakika kuhusu mustakabali wake Old Trafford, kwani kocha Ruben Amorim atalazimika kuuza baadhi ya wachezaji kabla ya kufanya usajili mpya majira ya joto. (Telegraph)

Bournemouth wameweka bei ya pauni milioni 45 kwa beki wao wa kushoto kutoka Hungary, Milos Kerkez mwenye umri wa miaka 21, ambaye anawaniwa na Liverpool. (iSport)

Kiungo wa kati wa Fulham, Tom Cairney, mwenye umri wa miaka 34, anawindwa na Wrexham walioelekea Championship, na huenda akapewa mkataba wa pauni 50,000 kwa wiki baada ya kuondoka Fulham kwa uhamisho wa bure. (Talksport)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’