Local,Normal News,Yanga, JKT

Yanga mikononi mwa JKT Tanzania, nusu fainali CRDB Cup

Joel JJ By Joel JJ
β€’
18 May 2025
Yanga mikononi mwa JKT Tanzania, nusu fainali CRDB Cup

Leo Jumapili, Mei 18, macho na masikio ya wapenda soka nchini yatakuwa mkoani Tanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani, ambako mabingwa watetezi Yanga SC watavaana na JKT Tanzania katika nusu fainali ya kwanza ya Kombe la CRDB.

Huu utakuwa ni mchezo wa tatu kwa timu hizi kukutana msimu huu. Yanga ilishinda mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC kwa mabao 2-0 kabla ya JKT Tanzania kuonyesha ubora wao na kuilazimisha Yanga sare tasa katika mchezo wa marudiano.

Kwa mantiki hiyo, pambano hili linatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku kila upande ukijivunia sababu za msingi kutaka kushinda.

Wananchi Watafuta Historia

Yanga SC wanasaka nafasi ya kutinga fainali ya Kombe la CRDB kwa mara ya tano mfululizo, wakitafuta kulinda heshima yao kama mabingwa watetezi wa taji hilo kwa misimu mitatu mfululizo.

Ushindi leo si tu utaendeleza rekodi yao nzuri, bali pia utawaweka katika nafasi ya kutetea taji lao kwa msimu wa nne mfululizo β€” jambo ambalo litakuwa la kihistoria katika soka la Tanzania.

Kocha Mkuu wa Yanga, Miloud Hamdi, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana, alithibitisha kuwa atashusha kikosi chake bora zaidi kuhakikisha anapata matokeo mazuri.

"Tunajua umuhimu wa mchezo huu, hatutaki kupoteza nafasi. Tutatumia wachezaji wetu muhimu kwa ajili ya kuhakikisha tunashinda na kufuzu fainali," alisema Hamdi.

JKT Tanzania wapambana kutengeneza Historia

Kwa upande wa JKT Tanzania, huu ni mchezo wao wa kwanza kabisa kufika hatua ya nusu fainali katika historia ya michuano hii. Hii ni nafasi ya dhahabu kwao kuandika historia mpya na kutinga fainali ya kwanza, huku ndoto ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) ikiwapeleka vitaniΒ 

Motisha kwa kikosi cha JKT Tanzania ni kubwa. Wameonyesha uimara wao msimu huu na wataingia dimbani kuwapa upinzani Yanga na pengine kuwashtua mabingwa hao watetezi.

Ratiba ya Mchezo

Mchezo huu wa kusisimua utapigwa saa 9:30 Alasiri kwenye uwanja wa Mkwakwani. Endapo dakika 90 za kawaida zitamalizika kwa sare, kutakuwa na dakika 30 za nyongeza, na iwapo bado mshindi hatapatikana, changamoto ya mikwaju ya penalti itaamua nani atatinga fainali.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’