Local,Transfer News,Yanga, Wydad

Aziz Ki atimkia Wydad Athletic

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 May 2025
Aziz Ki atimkia Wydad Athletic

Jana ilikuwa siku ya hisia kali kwa mashabiki wa Yanga SC – si tu kwa sababu ya ushindi mzuri wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania katika nusu fainali ya Kombe la CRDB, bali pia kwa heshima ya kipekee iliyotolewa kwa kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki.

Kupitia kitambaa cha unahodha alichovishwa, mashabiki na timu walionesha wazi kuwa huenda huu ukawa ulikuwa mchezo wake wa mwisho ndani ya jezi ya Yanga.

Aziz Ki, ambaye ni mfungaji bora na mchezaji bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu uliopita, anatarajiwa kujiunga na miamba wa soka kutoka Morocco, Wydad Athletic Club.

Taarifa za makubaliano kati ya Yanga na Wydad zilikuwepo kwa muda mrefu, zikisubiri tu hitimisho la msimu ili kuhalalisha safari ya kiungo huyo kwenda katika hatua nyingine ya mafanikio ya soka lake.

Kwa bahati mbaya, kuchelewa kumalizika kwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kumepelekea kuharakishwa kwa safari ya Aziz Ki, kwani Wydad wanajiandaa kwa michuano ya Kombe la Dunia la Klabu linalotarajiwa kufanyika Marekani kuanzia Juni 15.

Hii ina maana kuwa mechi zilizobakia za Ligi Kuu Aziz Ki hatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga

Katika misimu yake mitatu akiwa na Yanga, Aziz Ki ameacha alama isiyofutika: amekuwa kiungo wa ubunifu, mshambuliaji wa kuaminika, na kiongozi wa kipekee. Ametwaa makombe, ametengeneza mabao, na zaidi ya yote – amekuwa sehemu ya mafanikio ya Yanga

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’