International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi, May 22 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
22 May 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi, May 22 2025

Arsenal inataka kumnunua mshambuliaji wa Brazil Rodrygo, 24, ambaye anaweza kuondoka Real Madrid msimu huu wa joto. (Sky Germany)

Kiungo mshambuliaji wa Bayer Leverkusen Florian Wirtz anatarajiwa kuchagua kati ya kuhamia Bayern Munich na Liverpool ndani ya siku 10 zijazo, huku klabu zote zikiwa na hamu ya kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, 22. (Kicker - In Germany)

Barcelona wanataka kumsajili winga wa Liverpool mwenye umri wa miaka 28 kutoka Colombia Luis Diaz, ambaye amebakiza miaka miwili kwenye mkataba wake wa Anfield. (ESPN)

Liverpool wanamfuatilia winga wa Lyon na Ubelgiji Malick Fofana mwenye umri wa miaka 20 kama chaguo linalowezekana ikiwa Diaz ataihama klabu hiyo. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Napoli na Chicago Fire wanaongoza katika mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, 33, ambaye ataondoka Manchester City kama mchezaji huru msimu huu wa joto. (Sport)

Kiungo wa kati wa Manchester City James McAtee analengwa na Bayer Leverkusen, huku Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 22 pia akifuatiliwa na vilabu kadhaa vya Primia Ligi. (Sky Germany)

Chelsea wamedhamiria kumshikilia kiungo wa kati wa Argentina Enzo Fernandez, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kuwa kwenye orodha fupi ya Real Madrid ya wachezaji wanaoweza kuwindwa msimu huu. (Guardian)

Liverpool wamempa beki wao wa kati wa Uhispania Wellity Lucky, 19, mkataba mpya wa miaka minne. (Fabrizio Romano)

Rais wa Fiorentina Rocco Commisso anatazamiwa kukutana na mshambuliaji wa Italia Moise Kean kujaribu kumshawishi mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kusalia huku kukiwa na nia ya vilabu kadhaa. (Football Italia)

Viktor Gyokeres amewaambia wachezaji wenzake wa Sporting kuwa hana uhakika atacheza wapi mwaka ujao, huku mshambuliaji huyo wa Sweden mwenye umri wa miaka 26 akihusishwa na Arsenal na Manchester United. (Canal 11, via Star)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’