International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Jumamosi May 24 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
24 May 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumamosi May 24 2025

Nahodha wa Manchester United Bruno Fernandes atapewa muda hadi wiki ijayo kuamua kama anataka kuondoka katika klabu hiyo, huku Al Hilal wakipanga kutoa takriban Β£100m kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno, 30, ambaye angelipwa takriban Β£65m kwa msimu nchini Saudi Arabia. (Mirror)

Bayern Munich wanaweza kuanzisha mpango wa kumnunua Fernandes ingawa ada ya uhamisho ambayo United ingetaka inaweza kuwa kikwazo. (Teamtalk)

Winga wa Argentina Alejandro Garnacho, 20, ana uwezekano mkubwa wa kuondoka Manchester United msimu huu wa kiangazi baada ya kukatishwa tamaa na majukumu yake chini ya kocha mkuu Ruben Amorim. (ESPN)

Wawakilishi wa Garnacho wanatazamiwa kufanya mazungumzo na Manchester United kujadili mustakabali wa Muargentina huyo baada ya kuenguliwa kwenye fainali ya Ligi ya Europa dhidi ya Tottenham . (Telegraph - subscription required)

Kiungo wa kati wa Ujerumani Florian Wirtz, 22, angependelea kuhamia Liverpool badala ya Bayern Munich ikiwa ataondoka Bayer Leverkusen msimu huu wa kiangazi. (Subscription required)

Bayern Munich wanaamini kuwa winga wa Brighton na Japan Kaoru Mitoma, 28, ni mbadala wa Wirtz. (Sky Germany)

Everton wamefanya mazungumzo na mshambuliaji wa Ipswich na kikosi cha England cha vijana wenye chini ya umri wa miaka 21 Liam Delap, 22, kuhusu uhamisho wa majira ya kiangazi na pia wanavutiwa na winga wa Liverpool na Scotland Ben Doak, 19. (Guardian)

Real Madrid inamtazama kiungo wa kati wa Liverpool na Argentina Alexis Mac Allister kama mrithi wa asili wa mchezaji wa kimataifa wa Croatia Luka Modric, 39, ambaye anaondoka Bernabeu msimu huu wa joto. (Fichajes in Spanish )

RB Leipzig wamewasiliana na mkurugenzi mpya wa michezo wa Arsenal Andrea Berta kuhusu mpango unaowezekana wa kumuuza mshambuliaji wa Slovenia Benjamin Sesko, 21. (Sky Sports Germant - in Germany)

Mshambulizi wa Wolves na Brazil Matheus Cunha, 25, bado ana furaha kujiunga na Manchester United msimu huu wa kiangazi licha ya kushindwa kufuzu kwa soka la Ulaya msimu ujao. (Sky Sports)

Mlindamlango wa Aston Villa Emiliano Martinez, 32, anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo akiwa na timu za Saudi Pro League na Manchester United zinamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina. (teamTalk)

Aston Villa , West Ham na Leeds wanatazamia kumnunua kiungo wa kati wa Southampton na Ureno chini ya umri wa miaka 21 Matheus Fernandes, 20. (Football Insider)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’