Local,Normal News,Simba, Berkane

Fadlu awatisha RS Berkane

Joel JJ By Joel JJ
β€’
24 May 2025
Fadlu awatisha RS Berkane

Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids amesema licha ya ubora wa RS Berkane wamejipanga kutumia vyema uwanja wa nyumbani na kushinda mchezo wa mkondo wa pili fainali ya kombe la Shirikisho ambao utapigwa kesho Jumapili katika uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar

Akizungumza katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo, Fadlu alisema dhamira ya Simba ni kuona wanatwaa taji la Shirikisho (CAF CC) na kuandika histori mpya katika soka la Tanzania

Aidha amesema mechi ya kwanza ambayo walipoteza kwa mabao 2-0 nchini Morocco ilikuwa kama somo kwao hivyo wanafahamu namna ya kucheza mechi hiyo ya pili

"Tunafahamu Berkane ni timu ya daraja la juu barani Afrika kwa sasa lakini hawakukutana na Simba iliyo kwenye ubora na uwezo wake kamili"

"Tuko tayari kukabiliana nao na niseme tu, watakutana na hasira ya Simba. Mechi ya kwanza tumeitumia kama somo kuelekea mchezo huu wa pili," alisema Fadlu

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, nahodha msaidizi wa Simba Shomari Kapombe alisema walitamani mchezo huo upigwe katika uwanja wa Benjamin Mkapa lakini sasa kile ambacho walipanga kukifanya dimba la Mkapa, watakifanya hapo New Amaan Complex

"Tunafahamu kila mchezaji, Mwanachama na shabiki wa Simba alitamani mchezo huu upigwe uwanja wa Benjamin Mkapa lakini gatuwezi kupinga kilichoamuliwa na Mamlaka"

"Kile tulichopanga kukifanya uwanja wa Benjamin Mkapa, tutakifanya hapa uwanja wa New Amaan Complex," alisema Kapombe

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’