Local,Normal News,Simba, Singida

Simba yapania ushindi dhidi ya Singida BS

Joel JJ By Joel JJ
β€’
27 May 2025
Simba yapania ushindi dhidi ya Singida BS

Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola amesema wanahitaji kushinda mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida Black Stars hapo kesho ili kuhkikisha wanasalia katika mbio za ubingwa msimu huu

Akizungumza katika mkutano na wanahabari mapema leo, Matola alisema baada ya kikosi kurejea kutoka Zanzibar, moja kwa moja waliingia kambini kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya mchezo huo

Licha ya ugumu wa Singida Black Stars, Matola amesema ni matokeo ya ushindi pekee ambayo yatawabakisha katika mbio za ubingwa hivyo ni lazima washinde mchezo huo

"Sisi tuko tayari kwa mchezo huo, timu ilirejea salama kutoka Zanzibar na tunakamilisha maandalizi ya mchezo huu mgumu"

"Singida Black Stars ni moja ya timu ngumu msimu huu, ni timu imara ambayo ina wachezaji wengi wenye uzoefu mkubwa"

"Tulipokutana nao mara ya kwanza tulipata ushindi wa ao 1-0 ugenini lakini kila mmoja aliona jinsi mchezo ulivyokuwa mgumu"

"Lakini licha ya ugumu wao, kwetu sisi tunahitaji kushinda na tumejipanga kuondoka na alama zote tatu. Tunajua matokeo tofauti na ushindi yanaweza kuathiri malengo yetu ya kutwaa ubingwa msimu huu," alisema Matola

Simba na Singida Black Stars zitachuana katika mechi mbili zinazofuatana kwani baada ya mchezo wa ligi kuu, siku tatu baadae timu hizo zitachuana tena katika mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la CRDB ambao utapigwa uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Manyara May 31

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
44m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’