Local,Normal News,Simba, Singida

Dakika 180 za Simba mbele ya Singida BS

Joel JJ By Joel JJ
β€’
28 May 2025
Dakika 180 za Simba mbele ya Singida BS

Leo Jumatano, Mei 28, 2025, klabu ya Simba SC itashuka dimbani katika uwanja wa KMC Complex kuikabili Singida Black Stars kwenye mchezo wa ligi kuu ya NBC – mechi ya kiporo ambayo huenda ikaamua mwelekeo wa Simba katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Mchezo huu ni muhimu kwa Simba kushinda ili kusalia katika mbio za ubingwa wa ligi kuu msimu huu kabla ya mchezo dhidi ya Yanga SC uliopangwa kuchezwa Juni 15, 2025.

Baada ya mechi hii ya leo, Simba na Singida Black Stars watakutana tena siku tatu zijazo, Mei 31, 2025, katika nusu fainali ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, mjini Babati.

Hizi ni siku tatu zinazoweza kutafsiri hatima ya Simba msimu huu. Ushindi dhidi ya Singida leo unaweza kuwa chachu ya matumaini kwa Simba kuelekea mchezo mwingine mgumu wa nusu fainali ya Kombe la CRDB.

Unaweza kusema mechi hizi mbili dhidi ya Singida BS zinabeba matumaini ya Simba kushinda mataji makubwa yaliyobaki baada ya kulipoteza kombe la Shirikisho (CAF CC) lililochukuliwa na RS Berkane Jumapili iliyopita

Watani zao Yanga tayari wameshatinga fainali ya Kombe la CRDB baada ya kuifunga JKT Tanzania kwa mabao 2-0, na wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara, hii imeongeza presha kubwa kwa Simba kuhakikisha hawapotezi pointi leo.

Kwa Singida Black Stars, presha ni ndogo kwani tayari wamejihakikishia nafasi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao. Hata hivyo, watatumia mechi hizi kama fursa ya kuonyesha ubora wao na kujiimarisha zaidi kabla ya kampeni za kimataifa.

Macho yote yatakuwa KMC Complex na kisha kuelekea Babati – katika mechi muhimu kwa Simba kuhakikisha inakuwa na nafasi ya kushinda mataji msimu huu

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
1m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
30m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’