Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Hemed Morocco ametaja kikosi cha timu ya Taifa kitakachoelekea Afrika Kusini kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Bafana Bafana mchezo ambao uko katika kalenda ya FIFA
Aidha Stars imepata mwaliko wa kushiriki michuano ya COSAFA inayohusisha Mataifa ya kusini mwa Afrika
Akizungumza wakati anatangaza kikosi hicho, Morocco alibainisha kuwa baada ya mchezo dhidi ya Afrika Kusini Juni 06, wachezaji wanaozitumikia klabu za Simba na Yanga wataruhusiwa kurejea nchini kujiandaa na mchezo wa watani wa jadi utakaopigwa Juni 15 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Katika kikosi kilichotangazwa, Morocco amewajumuisha wachezaji 7 wa klabu ya Simba huku watatu wakitokea klabu ya Yanga
Wachezaji wa Simba ni Ali Salim, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Abdulrazak Hamza, Yusuph Kagoma, Valentino Mashaka na Kibu Denis
Mabeki Dickson Job na Ibrahim Bacca na kiungo mshambuliaji Shekhan Khamis wao wametokea klabu ya Yanga
