Singida BS yaifuata Yanga fainali CRDB Cup

Joel JJ By Joel JJ β€’ 31st May 2025


Singida BS yaifuata Yanga fainali CRDB Cup

Yanga itachuana na Singida Black Stars katika mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho la CRDB

Singida Black Stars imeifuata Yanga fainali leo baada ya kuifumua Simba mabao 3-1 katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Manyara

Jonathan Sowah na Emmenuel Keyekeh ndio waliopeleka kilio Msimbazi wakifunga mabao muhimu kwa timu yao Keyekeh akifunga mabao mawili

Bao pekee la Simba katika mchezo huo lilifungwa na Jean Charles Ahoua kupitia mpira wa adhabu

Yanga ilikuwa ya kwanza kutinga fainali ikiichapa JKT Tanzania mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa May 18


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.