Local,Normal News,Yanga, Simba

Yanga yaweka msisitizo, haitacheza Kariakoo Derby

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Jun 2025
Yanga yaweka msisitizo, haitacheza Kariakoo Derby

Yanga imeendelea kushikilia msimamo wake wa kutocheza mechi namba 184 ligi kuu ya NBC dhidi ya Simba hadi pale malalamiko yao yatakapofanyiwa kazi na mamlaka za soka nchini

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na mabingwa hao wa soka Tanzania Bara, mechi zilizobaki kuhitimisha msimu ni tatu tu

Juni 18 itacheza dhidi ya Tanzania Prisons (Ligi Kuu), Juni 22 dhidi ya Dodoma Jiji (Ligi Kuu) na mchezo wa mwisho ni fainali ya kombe la CRDB dhidi ya Singida Black Stars

Katika hatua nyingine, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amethibitisha kuwa timu hiyo imepokea mialiko ya kucheza mechi za kirafiki Rwanda na Kenya

"Ni kweli tuna mialiko miwili kutoka Rwanda na Kenya. Rayon Sports wametupa mwaliko kwenda kucheza nao mechi ya kirafiki lakini pia Gor Mahia wametualika Kenya"

"Uongozi unafanya tathmini na kutawataarifu mashabiki wetu wapi tunakwenda. Kama itakuwa Rwanda tutaandaa utaratibu wa safari kwa mashabiki pia"

"Hapo Rwanda tuna historia nafikiri wengi mnakumbuka tulichofanya miaka miwili iliyopita tulipokwenda kucheza na Al Merrikh," alisema Kamwe

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
3m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
32m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’