Fadlu ampigia hesabu kali Sowah

Joel JJ By Joel JJ β€’ 3rd June 2025


Fadlu ampigia hesabu kali Sowah

Kocha mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids, ameanza rasmi harakati za kuimarisha safu ya ushambuliaji kwa msimu ujao kwa kumtaja mshambuliaji hatari wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah, kama chaguo lake namba moja.

Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa tayari jina la nyota huyo limewasilishwa mezani kwa Rais wa heshima wa klabu hiyo, Bilionea Mohammed Dewji, kwa ajili ya kufanikisha usajili wake.

Hatua hii inaashiria mwanzo wa mbio kali za kuwania saini ya Sowah, ambaye msimu huu ameonesha kiwango cha juu akifunga mabao 11 katika mechi 12 za Ligi Kuu Tanzania Bara, na kuongeza idadi ya mabao kupitia mashindano ya Kombe la FA.

Uwezo wake wa kutumia nguvu, akili, na nafasi kwa ustadi mkubwa umemfanya kuwa mmoja wa washambuliaji wa kutazamwa kwa jicho la kipekee.

Juzi Sowah alifunga moja ya mabao ya Singida BS yaliyoizamisha Simba na kuitupa nje ya michuano ya kombe la CRDB ikifungwa mabao 3-1 katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa

Licha ya washambuliaji waliopo kikosini, Leonel Ateba na Steven Mukwala kufunga jumla ya mabao 24 msimu huu, Fadlu anaamini kuwa bado safu hiyo inahitaji mchezaji wa aina tofauti atakayewapa changamoto na kuongeza ushindani wa kweli.

Sowah anaonekana kuwa suluhisho linalowiana na mahitaji ya kiufundi ya Fadlu, hasa ukizingatia mfumo wake wa kushambulia kwa kasi na kutumia presha ya juu kuwalazimisha wapinzani kufanya makosa.

Mawasiliano Tayari Yameanza

Baada ya mechi mbili mtawalia ambazo Simba ilichuana na Singida BS, Fadlu alionekana kufanya mazungumzo na Sowah jijini Dar es salaam na hata baada ya mechi ya pili ya kombe la CRDB iliyopigwa Manyara

Mazungumzo hayo yamechukuliwa kama dalili ya wazi kuwa Fadlu anatamani kumuona Sowah akitua Msimbazi

Mwenyewe Sowah amefunguka kuwa yuko tayari kuitumikia tmu yoyote nchini hivyo atasubiri kuona kama kuna ofa itawasilishwa mezani


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.