Job kuongeza mkataba Yanga

Joel JJ By Joel JJ β€’ 3rd June 2025


Job kuongeza mkataba Yanga

Wiki iliyopita, klabu ya Yanga SC ilanza rasmi mazungumzo ya mkataba mpya na nahodha msaidizi wa timu hiyo, Dickson Job, ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Katika kikao kilichofanyika kati ya viongozi wa klabu hiyo na wawakilishi wa Job, imeelezwa kuwa makubaliano tayari yamefikiwa na wakati wowote Job ataongeza mkataba ambao utamuweka Jangwani hadi mwaka 2027.

Dickson Job anachukuliwa kama mmoja wa wachezaji wa msingi kabisa katika safu ya ulinzi ya Yanga, na mchango wake umeonekana wazi katika mafanikio ya timu hiyo msimu huu.

Yanga wamathibitisha bado wanahitaji huduma ya Job na hakuna shaka ataendelea kuwatumikia Wananchi


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.