Local,Normal News,Yanga, Simba, Azam, Fountain Gate, Singida BS

Mjumbe kamati ya saa 72 TPLB ajiuzulu

Joel JJ By Joel JJ
β€’
4 Jun 2025
Mjumbe kamati ya saa 72 TPLB ajiuzulu

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa vyanzo vya kuaminika, ni kwamba Ndugu George Mayawa, ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi maarufu kama Kamati ya Masaa 72, amejiuzulu

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Mayawa amechukua hatua hiyo baada ya kutoridhishwa kwake na mwenendo wa sasa wa uendeshaji wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Uamuzi huo umetajwa kuwa wa kimaadili na wenye lengo la kulinda hadhi ya mpira wa miguu nchini.

Mbali na nafasi hiyo, George Mayawa aliwahi pia kuhudumu katika Kamati ya Leseni za Klabu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), akiwa miongoni mwa wajumbe walioteuliwa katika awamu ya kwanza ya uongozi wa Rais Wallace Karia.

Hii ni hatua muhimu inayoashiria kuwepo kwa changamoto ndani ya mfumo wa uendeshaji wa ligi, na huenda ikawa chachu ya maboresho katika siku zijazo ingawa inaripotiwa kuwa kuna mengi ya kushangaza yanakuja siku za hivi karibuni.

Haya yanajiri wakati klabu ya Yanga ikishikilia msimamo wa kutocheza mechi dhidi ya Simba Juni 15 mpaka pale itakapopewa majibu kwa nini mchezo huo namba 184 haukufanyika March 08 tarehe iliyopangwa mwanzo

Yanga pia imeeleza kutokuwa na imani na baadhi ya viongozi wa Bodi ya Ligi ikiwataka Mtendaji Mkuu Almas Kasongo na Mwenyekiti Steven Mguto wawajibike

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
44m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’