Vurugu za mashabiki zaigharimu Simba

Joel JJ By Joel JJ β€’ 4th June 2025


Vurugu za mashabiki zaigharimu Simba

Vurugu za mashabiki wa Simba zilizojiri dimba la KMC Complex katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida Black Stars, zimeiponza Simba baada ya kupigwa faini ya Tsh Milioni 5 na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa ligi ya Bodi ya Ligi Kuu

Aidha Kamati hiyo pia imemfungia mechi tatu kocha wa viungo wa Simba Riedoh Berdien na kutozwa faini ya Tsh Milioni 1 kwa kocha la kuanzisha vurugu katika mchezo huo

Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids nae amepigwa faini ya Tsh Milioni 2 kwa kosa la kuishutumu Bodi ya Kuu Tanzania kuwa ina ajenda tofauti kuhusiana na ratiba ya michezo ya klabu hiyo kwenye Ligi Kuu ya NBC.

Fadlu alizungumza hayo alipokuwa anafanya mahojiano na Azam TV baada ya kumalizika kwa mchezo tajwa hapo juu, akionesha kutoridhishwa na ratiba ya michezo ya Ligi ya klabu yake.

Kamati pia imempiga faini ya Sh1 milioni mshambuliaji wa Singida BS Jonathan Sowah kwa kosa la kuwaonesha ishara ya matusi mashabiki wa klabu ya Simba waliokuwa jukwaani, pamoja na kitendo chake cha kung'oa kibendera cha kona.

Sowah aliyafanya makossa hayo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye uwanja wa KMC Complex kati ya timu yake dhidi ya Simba.

Mwamuzi Heri Sasii amefungiwa miezi sita kwa kosa la kushindwa kumudu mchezo huo baada ya kufanya maamuzi mengi yaliyoashiria kushindwa kutafsiri vema sheria 17 za mpira wa miguu kosa alilolifanya kwenye mchezo wa Simba v Singida Black Stars uliopigwa kwenye uwanja wa KMC, Simba ikishinda kwa bao 1-0.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.