Local,Normal News,Yanga, Simba

TPLB yafunguka maandalizi ya dabi

Joel JJ By Joel JJ
β€’
5 Jun 2025
TPLB yafunguka maandalizi ya dabi

Afisa Habari wa Bodi ya Ligi (TPLB) Karim Boimanda amesema maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu namba 184 kati ya Yanga dhidi ya Simba uliopangwa kupigwa Juni 15 katika uwanja wa Benjamin Mkapa yanaendelea vizuri

Boimanda amesema wadau wote wanaohusika na mchezo huo wanaendele na maandalizi huku Bodi ikihakikisha taratibu zote za msingi ili kufanikisha mchezo huo zinakamilika

Licha ya kauli za kutocheza mchezo huo zinazotoka upande wa Yanga, Boimanda amesema kama mwenyeji Yanga inawajibika kwa upande wake lakini bodi nayo itawajibika kwa upande wake pale wakati utakapowadia

Aidha kuhusu kutotangazwa kwa viingilio vya mchezo huo mpaka sasa, Boimanda amesema utaratibu wa viingilio ni uleule kwani viingilio vilivyotumika katika mchezo uliopaswa kupigwa March 08 ni vilevile kwa maana wale ambao walikata tiketi wakati ule watazitumia

"Maandalizi ya michezo mikubwa kama hii yako katika hatua mbalimbali, kwa sasa bado hatujafikia hatua ya kutaka kupata ripoti kutoka kwa timu mwenyeji ambaye anahusika kwa asilimia kubwa katika maandalizi likiwemo suala la viingilio"

"Kitu ambacho wadau wanapaswa kukumbuka ni kuwa mchezo huu ulishajadiliwa kuhusiana na viingilio vyake na tiketi zilianza kuuzwa na mpaka sasa ninapozungumza kuna tiketi zilinunuliwa na bado zipo kwenye kadi za mashabiki wetu wa zamani ambao walizinunua na tulishaeleza mara kadhaa tiketi zile hazijapotea zitatumika katika mchezo huu"

"Hakuna mjadala mkubwa kwenye suala la tiketi kwa sasa tunasubiri ufike wakati wa kutangaza kuendelea kuuza tiketi ambazo zilisitishwa baada ya mchezo ule kuahiridhwa"

"Tunaamini timu mwenyeji anaendelea na maandalizi yake kwa kuwa bado haujafikia wakati wa sisi kutaka kufahamu wamefikia wapi katika maandalizi hayo. Wakati utakapofika tutakuwa na vikao vyetu kupeana taarifa kuhusu maandalizi yote kwa ujumla," alisema Boimanda

Wakati taratibu za mchezo huo zikiendelea, viongozi wa Yanga wameendelea kushikilia msimamo kuwa Juni 15 hawatapeleka timu uwanjani

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’