Local,Normal News,Yanga, Simba

TPLB kufanyia kazi malalamiko ya Yanga, yasisitiza dabi ni Juni 15

Joel JJ By Joel JJ
β€’
9 Jun 2025
TPLB kufanyia kazi malalamiko ya Yanga, yasisitiza dabi ni Juni 15

Bodi ya Ligi Tanzania TPLB imesema katika mkutano wao na Yanga, klabu hiyo imekuja na mambo manne ambayo inataka yafanyiwe kazi kabla ya mchezo namba 184 uliopangwa kupigwa Jumapili Juni 15

Akitangaza hayo baada ya kikao kilichofanyika mapema leo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi Almas Kasongo amesema bodi yao imeyapokea na kwenda kuyafanyia kazi huku akisisitiza kwamba mchezo huo wa Juni 15, 2025 upo palepale

Kwenye hoja hizo Kasongo amezitaja kwamba Yanga imetaka Kamati ya usimamizi wa Ligi ivunjwe sambamba na kujiuzulu kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo.

Alisema pia Yanga imetaka Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF Wilfred Kidao naye ajizulu huku mwisho ikitaka Bodi ya Ligi iwe chombo huru

"Tumekutana na Yanga kilikuwa ni kikao kizuri chenye kujenga, kama mnavyofahamu TPLB ni chombo cha klabu na tunapokutana ni jambo lenye afya"

"Tumeyapokea mambo manne ambayo wameyaleta na sisi kama TPLB hatua ya kwanza tumeyapokea na baada ya kuyapokea tutakwenda kuyachakata"

"Kwenye haya mambo manne ni jambo moja ambalo lipo kwenye mamlaka ya Mwenyekiti wa Bodi ambalo ni muundo wa Kamati ya usimamizi wa Ligi lakini haya mengine yanahitaji muda na kuamuliwa kwenye vyombo vingine tofauti"

"Haya yanahitaji muda kuweza kupata muafaka wake hayawezi kufanyika kwa haraka hata kama ukitaka kuyafanyia kazi kwa hiyo kwa mamlaka yangu au wa nafasi yangu naweza kusema ratiba inabaki vilevile kama ambavyo ilipangwa mpaka hapo itakapoamuliwa vingine," alisemaa Kasongo

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
4m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
34m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’