International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi Juni 12 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 Jun 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi Juni 12 2025

Liverpool wako tayari kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa wa Paris St-Germain mwenye umri wa miaka 22, Bradley Barcola - hata baada ya kukamilisha dili la mshambuliaji wa Ujerumani wa Bayer Leverkusen, Florian Wirtz, 22. (Sun)

Aston Villa, Newcastle na Tottenham wanafuatilia maendeleo ya Jadon Sancho, 25, baada ya winga huyo wa Uingereza kurudi Manchester United kufuatia kumaliza kipindi chake cha mkopo pale Chelsea. (Sun)

Everton na Newcastle wanaongoza mbio za kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Jack Grealish, 29, kutoka Manchester City msimu huu wa joto. (Football Insider) Bayer Leverkusen wanataka kumsajili beki wa Liverpool Jarell Quansah, 22. (Athletic)

Mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez ana uwezekano mkubwa wa kuondoka Liverpool msimu huu wa joto, huku klabu ya Saudi Arabia Al-Hilal ikiwasiliana na Liverpool kuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 wiki hii. (Talksport)

Hata hivyo, Nunez anaeleweka kupendelea kubaki Ulaya, huku uhamisho kwenda Hispania au Italia ukiwa ndio chaguo lake la kwanza. (Mirror)

Athletic Bilbao wanatarajia kukubaliana na ongezeko la mshahara na mkataba mpya na winga wa Hispania Nico Williams, 22, ili kuzuia ushawishi kutoka Bayern Munich, Arsenal na Chelsea. (Marca)

Williams ameiambia Bayern kuwa yuko tayari kuhamia Ujerumani na uongozi wake upo kwenye mazungumzo na mabingwa hao wa Bundesliga. (Sky Sports Germany)

Winga wa Ujerumani Leroy Sane, 29, amekataa ofa kutoka Al-Hilal na amekubali kujiunga na Galatasaray baada ya mazungumzo kuhusu mkataba mpya na Bayern Munich kushindikana. (Sky Sport Germany)

Everton, Wolves na Fulham wanaangalia uwezekano wa kumsajili beki wa kulia wa Jamhuri ya Czech Vladimir Coufal, 32, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka West Ham. (Football Insider)

Nottingham Forest wanachuana na Leeds na Sunderland kumsajili beki wa kushoto wa Msumbiji Reinildo Mandava, 31, ambaye mkataba wake na Atletico Madrid unamalizika msimu huu wa joto. (Teamtalk)

Mshambuliaji wa Brazil Rodrygo, 24, anataka kubaki Real Madrid na kujiweka sawa chini ya kocha mpya Xabi Alonso. (Marca)

Real Betis wametoa ofa ya mkataba wa miaka mitatu kwa beki wa kushoto wa Jamhuri ya Dominika Junior Firpo, ambaye mkataba wake na Leeds unatarajiwa kumalizika, ingawa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 pia anazingatia ofa ya kubaki Elland Road na nyingine kutoka Lyon. (Mundo Deportivo)

Chelsea wamemuweka kipa wa Serbia Djordje Petrovic sokoni, huku Leeds wakiwa miongoni mwa vilabu vinavyovutiwa kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Teamtalk) Petrovic aliomba kutokuwemo kwenye kikosi cha Chelsea cha Kombe la Dunia la Klabu ili afuatilie masuala yake ya uhamisho. (Telegraph)

Manchester City wako karibu kufikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa Norway wa Rosenborg, Sverre Halseth Nypan, 18. (Athletic) Kiungo wa Argentina wa River Plate, Franco Mastantuono, 17, amekubali kujiunga na Real Madrid mwezi Agosti. (AS)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’