Local,Normal News,JKT, Simba

Bocco kuagwa kwa heshima JKT Tanzania

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 Jun 2025
Bocco kuagwa kwa heshima JKT Tanzania

Mshambuliaji wa JKT Tanzania, John Bocco imeelezwa huenda ukatumika mchezo dhidi ya Mashujaa utakaopigwa Juni 22, Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma kuagana na mashabiki wa timu hiyo.

Bocco alijiunga na timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Simba alikokuwa anafundisha timu ya vijana, licha ya kufunga mabao mawili akiwa na JKT Tanzania, ilielezwa sababu ya kupewa nafasi ya kuagana na mashabiki ni mchango wake kwa wachezaji wenzake, ikiwemo kuonyesha nidhamu ya hali ya juu katika majukumu aliyokuwa anayafanya.

β€œBocco amekuwa mfano wa kuigwa katika nidhamu ya kazi na mshauri kwa wachezaji ambao ni wadogo kwake namna ya kuhakikisha wanafanya kazi kwa kiwango cha juu kwa muda mrefu,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

β€œKila kitu Bocco anapenda kufanya kwa wakati na muda sahihi mfano kufika mazoezini, muda wa chakula, wakati mwingine bidii ya mazoezi yake binafsi ni kubwa kuliko wachezaji wanaojitafuta na wanaojitafuta wakiwa wameridhika.

β€œLicha ya mafanikio aliyonayo Bocco ya rekodi ya mabao mengi ya Ligi Kuu, maisha yake kiuchumi ila anavyopambana utadhani ndiyo anaanza kusaka maisha yake upya, nidhamu kwa kocha kiukweli wachezaji wanapaswa kujifunza mengi ili waweze kufanikiwa.”

Mwanaspoti

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
47m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’