Local,Normal News,Yanga

Mayay ajitosa Urais TFF

Joel JJ By Joel JJ
β€’
17 Jun 2025
Mayay ajitosa Urais TFF

Nyota wa zamani wa Yanga SC na Taifa Stars, Ally Mayay ametangaza rasmi nia ya kugombea Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti 16, 2025, jijini Tanga.

Mayay, anayejulikana kwa uzalendo wake, umahiri ndani na nje ya uwanja na ushawishi mkubwa katika mijadala ya soka kitaifa, anaingia kwenye mbio hizi akiwa na malengo ya kuleta mabadiliko makubwa kwenye uendeshaji wa mchezo huo.

Kwa muda mrefu, mashabiki na wadau wa mpira wamekuwa wakihitaji uongozi unaojali maendeleo ya mpira kuanzia ngazi za chini, na sasa Mayay anaonekana kujibu wito huo.

Licha ya kuwa kwenye kipindi kigumu cha maombolezo kufuatia kifo cha baba yake mzazi kilichotokea mkoani Tabora, leo saa 7 mchana, mwakilishi wake atachukua fomu ya kugombea kwa niaba yake, ishara ya dhamira thabiti ya kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi huo mkubwa wa kihistoria.

Hii itakuwa mara ya pili kwake kuchuana na Rais wa sasa wa TFF Wallace Karia kwani katika uchaguzi uliopita alichukua fomu lakini aliondolewa katika kinyang'anyiro kwa kigezo cha kutokuwa na cheti ya kidato cha nne licha ya kuwa Mayay ni msomi mwenye Shahada ya Uzamili ya Chuo Kikuu

Mayay si jina geni kwenye tasnia ya soka nchini. Mbali na kuichezea Yanga kwa mafanikio, amewahi kuitumikia timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kwa uzalendo mkubwa.

Baada ya kustaafu soka, amekuwa mchambuzi makini wa michezo, mtetezi wa wachezaji pia akiwa Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Tanzania

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’