Ukimya umeendelea kutawala katika kambi ya klabu ya Simba kuelekea mechi za kuhitimisha msimu wa 2024/2025 wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Licha ya kuonekana kutii maamuzi ya mamlaka, ni wazi uongozi wa Wekundu wa Msimbazi haujaridhishwa na mchakato wa kusogeza mbele mechi yao dhidi ya Yanga mechi ya Kariakoo Dabi ambayo sasa itapigwa Juni 25 badala ya Juni 15





