International,Transfer News,

Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi Juni 19 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Jun 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi Juni 19 2025

Mshambuliaji wa Sporting anayewaniwa na Arsenal na Manchester United Viktor Gyokeres, 27, amekataa kufanya mazungumzo ya wazi na kutishia kugoma huku akishinikiza kuondoka kwa klabu hiyo ya Ureno. (Mirror)

Fulham imekataa ofa ya pauni milioni 26, pamoja na nyongeza ya pauni milioni 6, kutoka kwa Leeds iliyopanda daraja kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Brazil Rodrigo Muniz, 24. (Standard)

Lakini Fulham wenyewe inafikiria kumsajili mshambuliaji wa PSV Eindhoven na Marekani Ricardo Pepi, 22, ambaye anafuatiliwa na klabu kadhaa za Uhispania na Italia. (Fabrizio Romano)

Beki wa Arsenal Myles Lewis-Skelly anakaribia kusaini mkataba mpya ambao utamfanya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 18 kuwa miongoni mwa wachezaji chipukizi wanaolipwa donge nono zaidi duniani. (Athletic - michango inahitajika)

Lakini meneja msaidizi Carlos Cuesta anatazamiwa kuondoka Arsenal ili kuchukua nafasi yake ya kwanza ya ukocha mkuu katika klabu ya Parma inayoshiriki ligi kuu ya Serie A. (Guardian)

Chelsea ina nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Morgan Rogers, 22, iwapo Aston Villa itakuwa tayari kumuachia. (Mail + - usajili unahitajika)

Liverpool iko tayari kuvunja rekodi ya uhamisho wa Uingereza kumsajili mshambuliaji wa Newcastle na Sweden Alexander Isak, 25, msimu huu wa kiangazi. (Give Me Sport)

Aston Villa iko tayari kumuuza kiungo wa kati Emi Buendia mwenye umri wa miaka 28 iwapo itapokea ofa ya zaidi ya Β£20m kwa Muargentina huyo. (Caught Offside)

Chelsea imefanya mawasiliano ya awali na Brighton kuhusu mshambuliaji wa Brazil Joao Pedro, 23, ambaye pia anasakwa na Newcastle. (Fabrizio Romano)

Brentford imeweka bei ya pauni milioni 50 kwa mshambuliaji Yoane Wissa, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa DR Congo akinyatiwa na Nottingham Forest, Tottenham, Arsenal, Fenerbahce na Galatasaray. (Team Talk)

Mshambuliaji wa Nice na Ivory Coast Evann Guessand, 23, anavutia klabu za Leeds na Tottenham, ambazo zimewasiliana na wawakilishi wa mchezaji huyo. (TBR Football)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’