Kiungo mshambuliaji wa Simba Jean Charles Ahoua ameandika rekodi mpya akiwa na Wekundu hao wa Msimbazi baada ya hapo jana kufunga bao na kutoa pasi ya goli wakati Simba ikiifumua KenGold mabao 5-0 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora
Aidha ameendelea kuongoza mbio za ufungaji bora akifikisha mabao 16 huku pia idadi ya pasi zake zilizosababisha mabao zikifika 9
Jumla sasa Ahoua amehusika katika mabao 25 yaliyofungwa na Simba msimu huu
Ahoua amevunja rekodi ya Clatous Chama msimu wa 2020/21 alipohusika katika mabao 24 akifunga mabao 10 na kutoa asist 14
Ikumbukwe huu ni msimu wa kwanza kwa Ahoua na dalili zinaonyesha anaweza kuwa mfungaji bora na hata mchezaji bora wa msimu 'MVP'