Local,Normal News,Yanga, Simba

Yanga vs Simba, kazi ipo ubingwa msimu huu

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Jun 2025
Yanga vs Simba, kazi ipo ubingwa msimu huu

Mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa mwaka 2025/26 kati ya Yanga na Simba zinazidi kunoga na lugha rahisi unayoweza kusema vita yao ni ng’adu kwa ng’adu kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Jana miamba hiyo yote ilikuwa ugenini, ambapo Yanga ilikuwa Uwanja wa Sokoine Mbeya ikicheza dhidi ya Prisons na kuibuka na ushindi wa mabao 0-5 huku Simba pia ikiwa ugenini Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora iliibuka na ushindi kama huo.

Kutokana na ushindi huo Yanga imefikisha pointi 76 kwa michezo 28, huku Simba nayo ikifikisha pointio 75 kwa michezo kama hiyo ya Yanga.

Timu hizo zote zimebakikisha mechi mbili, ambapo Jumapili wiki hii Simba itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar, huku Yanga ikiikaribisha Dodoma Jiji. Kisha Jumatano Juni 25, 2025 zitakutana zenyewe mechi yao ya kiporo iliyokuwa ichezwe Machi 8, 2025.

Azam nayo inashika nafasi ya tatu, huku pia ikipata ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Tabora United kwenye Uwanja wa Azam Complex na imefikisha pointi 60 ikiwa na mechi moja mkononi.

Singida Black Stars nayo ikaibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji ikiendelea kusalia nafasi ya nne ikifikisha alama 56

Fountain Gate inaelekea kwenda kucheza play-off ya kushuka daraja baada ya kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Coastal Union huku Tanzania Prisons nayo ikiwa hatarini kucheza play-off ikihitaji kushinda mchezo wake wa mwisho huku ikiomba Namungo Fc ipoteze mchezo wake wa mwisho pia

Prisons itahitimisha msimu ugenini kwa mchezo dhidi ya Singida BS wakati Namungo Fc itachuana na KenGold nyumbani

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’