Local,Normal News,Yanga, Simba, Azam, Fountain Gate, Singida BS

TPLB yajaza nafasi ya Mnguto, Kasongo

Joel JJ By Joel JJ
โ€ข
20 Jun 2025
TPLB yajaza nafasi ya Mnguto, Kasongo

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya mabadiliko muhimu katika safu yake ya uongozi kufuatia kuondoka kwa viongozi wawili wakuu, Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu waliotoka kwenye nafasi hizo kwa sababu tofauti mnamo Juni 13, 2025.

Katika hatua ya kuhakikisha utendaji wa bodi haukwami, TPLB imemteua Makamu Mwenyekiti wake, Nassor Idrissa โ€˜Fatherโ€™, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Azam FC, kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa bodi hiyo. Nafasi hiyo iliachwa wazi baada ya aliyekuwa Mwenyekiti, Steven Mnguto, kujiuzulu rasmi kwa barua mwishoni mwa juma lililopita.

Kwa upande mwingine, nafasi ya Mtendaji Mkuu wa TPLB imejazwa kwa muda na Ibrahim Mwayela, aliyekuwa Meneja Fedha wa bodi hiyo. Mwayela atakaimu nafasi hiyo kufuatia kusimamishwa kazi kwa Almas Kasongo na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia

Kupitia barua rasmi kwa klabu zote wanachama, TPLB ilieleza:

โ€œBodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) inakujulisha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Nassor Idrissa amekaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo kwa mujibu wa ibara 33:5 ya Kanuni za Uongozi za TPLB.

โ€œKatika hatua nyingine, Meneja Fedha wa TPLB, CPA Ibrahim Mwayela ameteuliwa kukaimu nafasi ya Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO), baada ya Almasi Kasongo kusimamishwa kazi mwishoni mwa juma lililopita. Bodi inatarajia ushirikiano wa dhati wa klabu yako kwa viongozi hao.โ€

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
46m ago
READ MORE โ†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE โ†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE โ†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE โ†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE โ†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE โ†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE โ†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE โ†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE โ†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE โ†’